Yawe wa majeshi anasema: Kisha nitawakaribia kwa kuwahukumu. Sitasita kutoa ushuhuda juu ya wachawi, wazinzi, watoa ushuhuda wa uongo, wanaopunja mushahara wa watumishi, wanaowatesa wajane na wayatima, wanaozuia mugeni asipate haki yake na wale wasioniogopa mimi.