Danieli 10:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
6 Mwili wake ulingaa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama ndimi za moto. Miguu na mikono yake ilingaa kama shaba iliyosafishwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya kundi kubwa la watu.
Mikono yake ni kama pete za zahabu, amevaa mawe ya bei kali. Kiwiliwili chake ni kama pembe za tembo zilizopambwa kwa mawe ya yakuti ya rangi ya samawi.
Vilipokuwa vinakwenda, nilisikia sauti ya mabawa yao; sauti ya muvumo huo ilikuwa kama ile ya maji mengi, kama sauti ya ngurumo kutoka kwa Mungu wa majeshi, na kama kelele ya jeshi. Viliposimama, vilikunja mabawa yao.
Basi, alinipeleka huko, nami nikamwona mutu aliyeonekana anaangaa kama shaba. Katika mikono yake mutu huyo alikuwa na kamba ya kitani ya kupima nayo pamoja na ufito wa kupima nao, naye alikuwa amesimama karibu na mulango.
Nilipoangalia, nikaona kitu kilichofanana na mwanadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alimetameta kama vile shaba.
Kisha nikaona malaika mwingine mwenye uwezo akishuka toka mbinguni. Alikuwa akifunikwa na wingu, naye alikuwa na upindi wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake ulingaa kama jua na miguu yake ilimetameta kama nguzo ya ndimi za moto.
Macho yake yalimetameta kama ndimi za moto, na juu ya kichwa chake kulikuwa taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa juu yake, wala hakuna mutu aliyejua, isipokuwa yeye mwenyewe tu.
“Umwandikie malaika wa kanisa la Tuatera hivi: “Ujumbe huu unatoka kwa Mwana wa Mungu, anayekuwa na macho yanayometameta kama ndimi za moto, na miguu inayongaa kama shaba iliyosafishwa vizuri sana.
wa tano wa mawe ya sadoniki, wa sita wa mawe ya akiki, wa saba wa mawe ya krisolite, wa nane wa mawe ya belulo, wa tisa wa mawe ya topazo, wa kumi wa mawe ya krisoparazo, wa kumi na moja wa mawe ya haikinto na wa kumi na mbili wa mawe ya amazito.