Waadui walipoondoka, wakamwacha akiwa ameumizwa vibaya sana, wakubwa wake wakamufanyia shauri baya, wakamwua juu ya kitanda chake, kwa kulipiza kisasi cha mauaji ya mwana wa kuhani Yoyada. Alizikwa katika muji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme.