1 Samweli 3:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
9 Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli: “Kwenda ulale, na akikuita, umwambie hivi: ‘Sema, ee Yawe, maana mimi mutumishi wako ninasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akarudi na kulala pahali pake.
Naye akamujibu: “Wala wenu wala wa waadui zenu! Lakini mimi ni jemadari wa jeshi la Yawe, na sasa nimefika.” Yoshua akainama chini kwa heshima, kisha akamwuliza: “Bwana wangu, unataka mimi mutumishi wako nifanye nini?”
Yawe akamwita Samweli kwa mara ya tatu. Samweli akaamuka, akamwendea Eli na kumwambia: “Nimekuja, maana umeniita.” Halafu Eli alitambua kwamba Yawe ndiye aliyemwita Samweli.