Wazao wa Isimaeli walikaa katika eneo lililokuwa kati ya Havila na Shuri, upande wa mashariki wa Misri, kuelekea Ashuri. Walikaa kwa utengano na wazao wengine wa Abrahamu.
Alikuwa na mali, kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, ngombe elfu moja, punda dike mia tano, na watumishi wengi sana. Yeye alikuwa wa heshima kuliko watu wote kule upande wa mashariki.
Kisha, Musa akawaongoza Waisraeli kutoka bahari Nyekundu, wakaenda mpaka kwenye jangwa la Suri. Wakasafiri kwa muda wa siku tatu katika jangwa bila kuona maji yoyote.
Sasa, uende kushambulia na kuangamiza vitu vyote wanavyokuwa navyo. Usiwaache wazima, lakini uwaue wote: wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wenye kunyonya, ngombe, kondoo, ngamia na punda.’ ”