Kisha, Yohana mwana wa Karea akazungumuza na Gedalia kwa siri kule Misipa, akamwambia: Uniruhusu niende nimwue Isimaeli mwana wa Netania, na hakuna mutu yeyote atakayejua. Kwa nini kumwachilia yeye akuue na Wayuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayuda waliobaki waangamie?