Nao Waisraeli waliokuwa upande wa pili wa bonde, na wengine waliokuwa upande wa mashariki wa muto Yordani walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, naye Saulo na wana wake wamekufa, waliihama miji yao, wakakimbia. Wafilistini wakaenda na kukaa katika miji hiyo.