Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


143 Mistari ya Biblia kuhusu Utii kwa Amri

143 Mistari ya Biblia kuhusu Utii kwa Amri
Yohana 14:15

“Mkinipenda mtazishika amri zangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:1-17

Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, Lakini siku ya saba ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala watumishi wako wa kike, wala mnyama wako wa kufugwa, wala mgeni aliye nyumbani mwako. Maana kwa siku sita mimi Mwenyezi-Mungu niliziumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo, kisha nikapumzika siku ya saba. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu niliibariki siku ya Sabato, nikaitakasa. “Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. “Usiue. “Usizini. “Usiibe. “Usimshuhudie jirani yako uongo. “Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 6:5-6

Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu zenu zote. Wekeni mioyoni mwenu maneno hayo ninayowaamuru leo

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 22:37-40

Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote’. Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe’. Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa: Karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ndama wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari; njoni harusini.’ Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:10

Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:9

Kijana atatunzaje maisha yake kuwa safi? Kwa kuyaongoza kadiri ya neno lako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:3

maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 10:12-13

“Sasa, enyi Waisraeli, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anataka nini kwenu, ila kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote, kumpenda, kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote, na kuzitii amri na masharti ya Mwenyezi-Mungu ninayowawekea leo, kwa manufaa yenu wenyewe?

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoshua 1:8

Hakikisha kuwa hutakisahau kamwe kitabu hiki cha sheria; bali kila siku utajifunza kitabu hiki, mchana na usiku, ili upate kutekeleza yote yaliyoandikwa humu, nawe utafanikiwa na kustawi popote uendapo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:2

Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote,

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:21

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:1-2

Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Hapo ghala zako zitajaa nafaka, na mapipa yako yatafurika divai mpya. Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi. Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu. Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu. Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu; kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima. Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Samueli 15:22

Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:21

Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:22

Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 26:3-4

“Kama mkifuata masharti yangu na kuzishika amri zangu, Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa. Miji yenu nitaiteketeza mahali penu patakatifu nitapafanya jangwa na harufu zenu nzuri za sadaka kamwe sitazikubali. Nitaiteketeza nchi yenu hivyo kwamba hata adui wanaohamia humo watashangaa. Nitawatawanya nyinyi miongoni mwa watu wa mataifa na kuchomoa upanga dhidi yenu. Nchi yenu itakuwa ni ukiwa na miji yenu uharibifu. “Nyinyi mtakapokuwa mikononi mwa adui zenu, hapo ndipo nchi itakapozifurahia sabato zake wakati itakapokuwa hali ya ukiwa. Nchi itapumzika na kufurahia sabato zake. Kadiri itakapokuwa hali ya ukiwa itapata kiasi ambacho haikupata katika sabato zenu mlipokuwa mkiishi humo. Na kwa baadhi yenu watakaosalimika nitawaletea woga mioyoni mwao, katika nchi ya adui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mtu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hamna mtu anayewafukuza. Wataangukiana ovyo kama mtu anayekimbia vita hata kama hamna anayewafukuza. Hamtakuwa na nguvu yoyote kuwakabili adui zenu. Mtaangamia kati ya mataifa na nchi za adui zenu zitawameza. Kama baadhi yenu wakisalimika katika nchi za adui zenu watadhoofika kwa sababu ya uovu wao; na kwa sababu ya uovu wa wazee wao. nitawanyeshea mvua wakati ufaao, nchi ipate kuzaa mavuno kwa wingi, nayo miti ya mashambani matunda yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 6:16

Mnajua kwamba mkijitolea nyinyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo – au watumwa wa dhambi na matokeo yake ni kifo, au wa utii na matokeo yake ni kufanywa kuwa waadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:24

Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 11:1

“Kwa ajili hiyo, mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika siku zote kanuni zake, masharti yake, maagizo yake na amri zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:22

Lakini mkimsikiliza kwa makini na kufanya yote asemayo, mimi nitakuwa adui wa adui zenu na mpinzani wa wapinzani wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 128:1

Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 11:26-28

“Angalieni, leo hii nawawekea mbele yenu baraka na laana: Baraka, kama mtatii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo nawapeni hivi leo; na laana, kama hamtazitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuiacha njia ninayowaamuru, mkaabudu miungu mingine ambayo hata hamjawahi kuijua.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 13:34-35

Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 2:3

Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 10:17

Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:11

Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 5:9

Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii,

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Yohana 1:6

Upendo maana yake ni kuishi kwa kuzitii amri zake Mungu. Amri mliyoisikia tangu mwanzo ndiyo hii: Mnapaswa nyote kuishi katika upendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 7:19

Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilicho muhimu ni kuzishika amri za Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 5:29

Laiti wangekuwa daima na mawazo kama haya wakaniheshimu na kushika amri zangu! Mambo yao yote yangewaendea vyema daima wao wenyewe na wazawa wao milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:19

Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 4:40

Kwa hiyo shikeni masharti yake na amri zake ambazo ninawapeni leo ili mfanikiwe, nyinyi pamoja na wazawa wenu, na kuishi siku nyingi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni iwe yenu milele.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 112:1

Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:46

“Mbona mwaniita ‘Bwana, Bwana,’ na huku hamtimizi yale ninayosema?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:44

Nitatii sheria yako daima, nitaishika milele na milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:2

Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:12-13

Wapenzi wangu, nilipokuwa nanyi mlinitii daima, na hata sasa niwapo mbali nanyi endeleeni kutii. Fanyeni kazi kwa hofu na tetemeko kwa ajili ya ukombozi wenu, kwani Mungu ndiye afanyaye kazi daima ndani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mpango wake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 13:4

Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 15:26

akawaambia, “Ikiwa mtaisikiliza kwa makini sauti yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kutenda yaliyo sawa mbele yangu, na kuheshimu amri na maagizo yangu yote, basi, mimi sitawaletea yale magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa sababu, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewaponya nyinyi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:60

Bila kukawia nafanya haraka kuzishika amri zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:17

Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:13

Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:105

Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 28:1-2

“Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani. Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa. Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni, Mwenyezi-Mungu atawafungulieni hazina yake nzuri kutoka mbinguni na kunyesha mvua katika nchi kwa wakati wake, na kubariki kazi zenu. Mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza, bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia. “Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote: Mtapata laana katika miji yenu na mashamba yenu. Vikapu vyenu vya nafaka vitalaaniwa na vyombo vyenu vya kukandia mkate. Watoto wenu watalaaniwa na mazao yenu ya nchi; mifugo yenu italaaniwa isiongezeke. Mtalaaniwa mnapoingia na mnapotoka. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo;

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 8:31

Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 12:13

Baada ya hayo yote yaliyokwisha semwa bado kuna hili linalotakiwa: Mche Mungu, na uzishike amri zake; kwa sababu hilo ndilo jukumu aliloumbiwa binadamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:8

Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa, huufurahisha moyo; amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi, humwelimisha mtu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:3

Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 11:28

Lakini Yesu akasema, “Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:34

Unieleweshe nipate kuishika sheria yako, niifuate kwa moyo wangu wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:1

Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 30:16

Kama mkitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo ninawapa leo, mkampenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake na kushika masharti na maagizo yake, basi, mtaishi na kuongezeka; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:14-15

Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga. Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:1

Heri watu wanaoishi bila kosa, wanaozingatia sheria ya Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 13:13

Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi, lakini anayetii amri atapewa tuzo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 2:10

Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 10:5

na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu; tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 7:9

Basi, jueni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayeshika agano lake na huwaonesha fadhili kwa vizazi vingi vya wale wanaoshika amri zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:11

Yanifunza mimi mtumishi wako; kuyafuata kwaniletea tuzo kubwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:35

Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo napata furaha yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 28:20

Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:22

na kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:23

Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 8:6

Hivyo, shikeni amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpate kuzifuata njia zake na kumcha yeye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:6

Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:100

Nawapita wazee kwa busara yangu, kwa sababu nazishika kanuni zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:5

Laiti mwenendo wangu ungeimarika, kwa kuyafuata masharti yako!

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wafalme 17:13

Mwenyezi-Mungu alituma manabii na waonaji kuionya Israeli na Yuda akisema, “Acheni njia zenu mbaya mkatii amri zangu na maagizo yangu kufuatana na sheria nilizowapa babu zenu, na ambazo niliwapeni kupitia kwa watumishi wangu manabii.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 32:46-47

aliwaambia, “Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo ninawapeni leo. Lazima muwaamuru watoto wenu ili wafuate kwa uaminifu maneno yote ya sheria hii. Maana sheria hii si maneno matupu bali ni uhai wenu; kwa sheria hii mtaishi maisha marefu katika nchi mnayokwenda kuimiliki, ngambo ya mto Yordani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:17-19

“Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha. Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia. Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 1:19

Mkiwa tayari kunitii, mtakula mazao mema ya nchi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:66

Unifundishe akili na maarifa, maana nina imani sana na amri zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 3:12

Maana Bwana huwatazama kwa wema waadilifu na kuzisikiliza sala zao. Lakini huwapa kisogo watu watendao maovu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:14

Nyinyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 19:5

Sasa basi, kama mkiitii sauti yangu na kulishika agano langu, mtakuwa watu wangu wateule kati ya mataifa yote, maana dunia yote ni yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 1:1-2

Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, na kuitafakari mchana na usiku.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 11:27-28

Baraka, kama mtatii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo nawapeni hivi leo; na laana, kama hamtazitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuiacha njia ninayowaamuru, mkaabudu miungu mingine ambayo hata hamjawahi kuijua.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 24:7

Kisha akachukua kitabu cha agano la Mwenyezi-Mungu, akakisoma mbele ya watu, nao wakasema, “Hayo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya, nasi tutakuwa watiifu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 3:14

Tena kama ukifuata njia na maagizo yangu na kushika amri zangu kama alivyofanya baba yako Daudi, basi, nitakupa maisha marefu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:48

Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 6:17

Hakikisheni kwamba mnazitii amri zake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, maamuzi na masharti yake ambayo amewaamuru.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:128

Kwa hiyo, nafuata kanuni zako zote; kila njia potovu naichukia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:4

Baba yangu alinifundisha hiki: “Zingatia kwa moyo maneno yangu, shika amri zangu nawe utaishi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 19:8

Watu wote wakaitikia kwa pamoja wakisema, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.” Mose akamjulisha Mwenyezi-Mungu jibu hilo la watu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:173

Uwe daima tayari kunisaidia, maana nimeamua kufuata kanuni zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 10:27

Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 7:12

Basi, sheria yenyewe ni takatifu, na amri yenyewe ni takatifu, ni ya haki na nzuri.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:10

Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:58

Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 16:28

Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mpaka lini mtakataa kuzitii amri na Sheria zangu?

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:4

Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 4:2

Msiongeze chochote katika amri ninazowapeni, wala msipunguze kitu; zingatieni amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo ninawapeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 19:17

Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:40

Natamani sana kuzitii kanuni zako; unijalie uhai maana wewe ni mwadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 4:25-32

Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo. Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima. Msimpe Ibilisi nafasi. Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini. Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu. Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu. Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni. Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu! Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:7

Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu, humpa mtu uhai mpya; masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:36

Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:13

Yazingatie yote niliyokuambia. Usiyataje hata kidogo majina ya miungu mingine; hayo yasisikike kinywani mwako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:4

Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:106

Nimeapa na kuthibitisha kiapo changu, kwamba nitashika maagizo yako adili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:14

Maana sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 5:32-33

“Nyinyi muwe waangalifu mkafanye kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru; tekelezeni kila kitu barabara. Mtafuata njia yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata ili mambo yenu yawaendee vyema na mpate kuishi muda mrefu katika nchi mtakayotwaa iwe mali yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:20

Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:47

Furaha yangu ni kuzitii amri zako, ambazo mimi nazipenda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:24-27

“Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba. “Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena anguko hilo lilikuwa kubwa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:3

“Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:57

Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe riziki yangu kuu; naahidi kushika maneno yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 2:8

Kama mnaitimiza ile sheria ya ufalme kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe”, mtakuwa mnafanya vema kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:168

Nazingatia kanuni na maamuzi yako; wewe wauona mwenendo wangu wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Samueli 15:22-23

Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu. Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli, na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago. Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 8:32-33

“Sasa basi wanangu, nisikilizeni: Heri wale wanaofuata njia zangu. Sikilizeni mafunzo mpate hekima, wala msiyakatae.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:33

Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 27:10

Kwa hiyo mtatii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu mkizifuata amri zake na masharti yake ambayo ninawaamuru leo.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:88

Unisalimishe kadiri ya fadhili zako, nipate kuzingatia maamuzi uliyotamka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:9

Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:12

Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:2

Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:101

Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoshua 22:5

Muwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mfuate anachotaka na kushika amri zake; mkae pamoja naye na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:1-3

Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara. Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama mkanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu. Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Injili kwa uthabiti. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, Mimi ni balozi kwa ajili ya Injili hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo. Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya. Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo. Ninawatakieni nyinyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho. “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 7:2

Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:97

Naipenda sana sheria yako! Naitafakari mchana kutwa!

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:47-49

Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza: Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara. Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 6:14

nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 31:12-13

Wakusanye watu: Wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili kila mmoja asikie maneno haya ya kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuwa waangalifu kutekeleza maneno ya sheria hii. Nao wazawa wao ambao hawajasikia sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, wapate kuisikia na kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, muda wote mtakaoishi katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki ngambo ya mto Yordani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:2

Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Mambo ya Nyakati 28:8

“Basi sasa, mbele ya kusanyiko hili la Waisraeli wote, jumuiya ya watu wa Mwenyezi-Mungu, na mbele ya Mungu wetu, angalieni mzishike amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ili mwendelee kuimiliki nchi hii nzuri, na kuwarithisha wazawa wenu baada yenu, hata milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:174

Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 15:3-9

Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe? Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya. Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; watu wakamsifu Mungu wa Israeli. Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, “Nawaonea huruma watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende zao bila kula, wasije wakazimia njiani.” Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?” Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba na visamaki vichache.” Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu. Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu saba. Hao waliokula walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto. Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la Magadani. Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’ Lakini nyinyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema: ‘Kitu hiki nimemtolea Mungu,’ basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe. Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu: ‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:5

Kwa njia yake, mimi nimepewa neema ya kuwa mtume, ili kwa ajili yake niwaongoze watu wa mataifa yote wapate kuamini na kutii.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:111

Maamuzi yako ni riziki kubwa kwangu milele; hayo ni furaha ya moyo wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:24

Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 30:10

ikiwa mtiatii sauti yake na kushika amri na masharti yake yaliyoandikwa katika kitabu hiki cha sheria na kumrudia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wote na roho yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:4

Ee Mungu, umetupatia kanuni zako ili tuzishike kwa uaminifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 4:17

Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:10-11

Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:102

Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 19:16

Anayeshika amri anasalimisha maisha yake; anayepuuza agizo atakufa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 1:10

Kwa hiyo basi, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuufanya huo wito wenu mlioitiwa na Mungu uwe jambo la kudumu katika maisha yenu; kama mkiishi namna hiyo hamtaanguka kamwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:32

Nitafuata maelekezo ya amri zako, maana unanipa maarifa zaidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 5:10

Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 8:31-32

Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu. Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Tufuate:

Matangazo


Matangazo