Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


113 Mistari ya Biblia kuhusu Uasherati

113 Mistari ya Biblia kuhusu Uasherati

Biblia inatufunza kuepuka uovu wa kila aina na kutenda mema wakati wote. Uasherati, iwe ni kwa matendo au mawazo, unatutenga na njia za Mungu na kutupeleka kwenye njia hatari.

Mithali 6:32-33 inatuonya kuhusu madhara ya uasherati: "Mtu aziniye na mwanamke hana akili; mtu afanyaye hivyo hujiangamiza nafsi yake. Atapata mapigo na fedheha; aibu yake haitafutwa." Maneno haya yanatuonyesha uzito wa matendo ya uasherati na jinsi yanavyoathiri maisha yetu ya kiroho na mahusiano yetu.

Ni muhimu kukumbuka kwamba uasherati siyo tu matendo yetu, bali pia mawazo na tamaa zetu za ndani. Yesu alitufundisha katika Mathayo 5:28: "Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amtazameye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake." Neno hili linatuonyesha jinsi tunavyopaswa kutubu kwa kina na kutafuta usafi katika kila nyanja ya maisha yetu.

Tunapofikiria kuhusu uasherati, ni muhimu kuishi kwa kutii amri za Mungu. Tunapaswa kuacha kila kitu kinachotutenga na mapenzi yake na kutafuta utakatifu katika kila kitu tunachofanya na kufikiria. Ni kwa njia hii tu ndipo tunaweza kupata utimilifu wa maisha katika ushirika na Mungu na kuepuka madhara ya uharibifu ya uasherati.


1 Wakorintho 7:2

lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:3-5

Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa. Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 6:18

Jiepusheni kabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zote hutendwa nje ya mwili lakini mzinzi hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:1

Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:19-21

Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: Uzinzi, uasherati, ufisadi; Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote. kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: Watu wanaotenda mambo hayo hawataupata ufalme wa Mungu uwe wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:3

Kwa vile nyinyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:3

Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 19:9

Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:27-28

“Mmesikia kwamba watu waliambiwa: ‘Usizini!’ Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 5:3-5

Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 6:9

Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:19

Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: Uzinzi, uasherati, ufisadi;

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:11

Nilichoandika ni hiki: Msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi, mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:32

Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 9:21

Wala hawakutubu na kuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:26-27

Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke, wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 2:22

Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 2:21

Nimempa muda wa kutubu, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 12:21

Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 10:8

Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:10

Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu nyinyi kuihama dunia hii kabisa!

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 6:32

Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa; huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:9

Niliwaandikia katika barua yangu msishirikiane na wazinzi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:4

Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:16

Jihadharini ili miongoni mwenu pasiwe na mtu mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, aliyeuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mlo mmoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 2:24

Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 22:15

Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 1:10

sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wezi wa watu, waongo na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho sahihi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 18:22

“Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:13-14

Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 4:19

Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 6:25-26

Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya, lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai wako wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:7

Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:5

Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia: Uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 15:19

Maana moyoni hutoka mawazo ya uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 6:12-13

Kwa hiyo, dhambi isiitawale tena miili yenu ambayo hufa, na hivyo kuzitii tamaa zake. Wala msitoe hata sehemu moja ya miili yenu iwe chombo cha kutenda uovu na dhambi. Badala yake, jitoleeni nyinyi wenyewe kwa Mungu kama watu waliofufuliwa kutoka kwa wafu; toeni nafsi zenu zote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:11-12

Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:16

Vitu vyote vya ulimwengu – tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali – vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:16-17

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 6:13

Unaweza kusema: “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula.” Sawa; lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mtu si kwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili ya kumtumikia Bwana, naye Bwana ni kwa ajili ya mwili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 19:4-6

Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke, na akasema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’ Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 20:13

Kama mwanamume yeyote akilala na mwanamume mwenzake kana kwamba ni mwanamke, basi, wote wawili ni lazima wauawe kwani wamefanya jambo lililo chukizo; watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:14

“Usizini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 7:21-23

Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza; kijana akashawishika kwa maneno yake matamu. Hapo akamfuata huyo mwanamke moja kwa moja, kama ng'ombe aendaye machinjioni, kama paa arukiaye mtegoni. Hakutambua kwamba hiyo itamgharimu maisha yake, mpaka alipojikuta amekuwa kama amechomwa mshale moyoni, amekuwa kama ndege aliyenaswa wavuni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yuda 1:7

Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:5

Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 2:23

Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima kwa namna ya ibada wanayojishurutishia, unyenyekevu, na kuutendea mwili kwa ukali; lakini hayafai chochote kuzuia tamaa za mwili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:6-8

Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uhai na amani. Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii. Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:23

Linda moyo wako kwa uangalifu wote, maana humo zatoka chemchemi za uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:15-16

Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:8

Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:3-4

Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu. Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 5:18-19

Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa. Mahaba yake yakufurahishe kila wakati, umezwe daima na pendo lake.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 6:19-20

Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe. Je, hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi, ulimwengu utahukumiwa nanyi, kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika mambo madogo? Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:8

Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 1:9

Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 6:14

Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 7:25-27

Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo, wala msipitepite katika mapito yake. Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, ni mahali pa kuteremkia mautini.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:11

Wapenzi wangu, nawasihi nyinyi kama wageni na wakimbizi hapa duniani! Achaneni na tamaa za mwili ambazo hupingana na roho.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 13:4-5

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:11

Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 51:10

Uniumbie moyo safi, ee Mungu, uweke ndani yangu roho mpya na thabiti.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 23:26-27

Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Malaya ni shimo refu la kutega watu; mwanamke mgeni ni kama kisima chembamba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:1-2

Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana. Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia. Ishini kwa kupatana vema nyinyi kwa nyinyi. Msijitakie makuu, bali jishughulisheni na madogo. Msijione kuwa wenye hekima sana. Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote. Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote. Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.” Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:24

Wale walio na Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 5:22

Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:3

Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:24-25

Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao. Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:30

Madaha huhadaa na uzuri haufai, bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:2

Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 3:3-4

Katika kujipamba kwenu msitegemee mambo ya njenje, kama vile mitindo ya kusuka nywele, kujivalia vitu vya dhahabu na nguo maridadi. Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:22

na kuepuka kila aina ya uovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:26-27

Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna tambiko iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi. Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 4:24

Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:10

hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni wakaidi na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:7

Waovu na waache njia zao mbaya, watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya; wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia, wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:12-14

Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga. Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 6:15-17

Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo! Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye – kama ilivyoandikwa: “Nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Lakini aliyejiunga na Bwana huwa roho moja naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 5:1-2

Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni. Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu, wala kuwategea sikio wakufunzi wangu. Sasa niko karibu kuangamia kabisa mbali na jumuiya ya watu.” Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Hiyo ni yako wewe mwenyewe, wala usiwashirikishe watu wengine. Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa. Mahaba yake yakufurahishe kila wakati, umezwe daima na pendo lake. Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara, na midomo yako izingatie maarifa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 19:5-7

Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.” Loti akatoka nje, akafunga mlango nyuma yake, akawaambia, “Ndugu zangu, nawasihi msitende uovu huo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:1-4

Endeleeni kupendana kindugu. Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi hawana haki ya kula vitu vyake. Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji. Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake. Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu. Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu. Mtuombee na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima. Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo. Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua. Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina. Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni. Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu. Wasalimuni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni. Tunawatakieni nyote neema ya Mungu. Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao. Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 22:14

Kinywa cha mwasherati ni shimo refu; anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:13

Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [ Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 7:5-6

Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya, vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni. Siku moja dirishani mwa nyumba yangu, nilichungulia nje kupitia viunzi vya dirisha,

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 101:3

sitavumilia kamwe upuuzi. Nayachukia matendo ya watu wapotovu, mambo yao hayataambatana nami.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 11:34

Jicho lako ni taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:30

Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 2:3

Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:37

Uniepushe, nisifuate mambo ya upuuzi; unioneshe njia yako, unipe uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 1:3-4

Kwa uwezo wake wa kimungu, Mungu ametujalia mambo yote tunayohitaji ili tuishi maisha ya kumcha Mungu kwa kumjua yeye aliyetuita tuushiriki utukufu na wema wake yeye mwenyewe. Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 9:13-18

Mwanamke mpumbavu ana kelele, hajui kitu wala hana haya. Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake, huweka kiti chake mahali pa juu mjini, na kuwaita watu wapitao njiani, watu wanaokwenda kwenye shughuli zao: “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: “Maji ya wizi ni matamu sana; mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.” Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu, wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 4:12

Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: Katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 16:19

Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:33

Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:15-16

ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga, mkishika imara ujumbe wa uhai. Na hapo ndipo nami nitakapokuwa na sababu ya kujivunia katika siku ile ya Kristo, kwani itaonekana dhahiri kwamba bidii yangu na kazi yangu havikupotea bure.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 5:17

Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:13

Kwa maana, kama mkiishi kufuatana na matakwa ya maumbile ya kibinadamu, hakika mtakufa. Lakini, kama kwa njia ya Roho mnayaua matendo yenu maovu, basi, mtaishi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:133

Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 22:37-39

Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote’. Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe’.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:23

Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu – roho, mioyo na miili yenu – mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:101

Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 8:13

Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu. Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya; nachukia na lugha mbaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 1:16-17

Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu. Acheni kutenda maovu, jifunzeni kutenda mema. Tendeni haki, ondoeni udhalimu, walindeni yatima, teteeni haki za wajane.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:18

Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:14

Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 9:27

Naupa mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:14-15

Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga. Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:4-5

Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 7:9

Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia, basi na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:1-2

Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana nyinyi ni watoto wake wapenzi. Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Lakini kila kitu kikifichuliwa na mwanga, ukweli wake hudhihirishwa; na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: “Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangaza.” Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. Upendo uongoze maisha yenu kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama tambiko yenye harufu nzuri na sadaka impendezayo Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Baba Mungu wa mbinguni, asante kwa kunipa siku hii mpya ya uzima. Asante kwa upendo wako na rehema zako kwangu. Asante kwa kuwa nami na kwa kujidhihirisha katika udhaifu wangu. Asante kwa uaminifu wako na kwa kuniosha dhambi zangu zote. Kwa mara nyingine tena naomba damu ya thamani ya Yesu initakase. Nakuja mbele zako nikijua nimekosa. Tamaa iliyo ndani yangu hunisukuma kufanya yasiyofaa mbele zako. Sitaki kuongozwa na hisia zangu tena. Nataka nifinyangwe kwa mfano wako, nisiwe na uovu wowote ndani yangu. Kwa hivyo nakuomba Yesu unioshe uchafu wote. Nyosha njia zangu nisipotee. Niongoze kwenye kweli yako, na neno lako linikaripie ninapokosea katika mawazo yangu. Safisha akili yangu, roho yangu na nafsi yangu, niwe harufu nzuri mbele zako. Katika jina la Yesu, Amina.
Tufuate:

Matangazo


Matangazo