Mithali 18:21 inatufunza kwamba maneno yetu yana nguvu sana. Tunaweza kuyatumia kutangaza uzima au kifo. Kwa hivyo, ni muhimu tuyatumie kubariki badala ya kulaani, tukiwa mfano wa Mungu hapa duniani.
Kumbuka kifo ni hakika, kwa hivyo ni muhimu kuishi kila siku kwa uwajibikaji na bidii. Yesu anatuita kwa mambo makuu, basi tutembee naye, katika nuru wala si gizani.
Mungu anataka tuwe waangalifu na maneno yetu, kwani yana uwezo wa kuleta mambo katika ulimwengu huu. Tuamue kutembea na Yesu, ambaye ni uzima, wala si katika dhambi zinazoongoza kwenye kifo.
“Nawe Yeremia utawaambia watu hawa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sikilizeni! Mimi nawapeni nafasi ya kuchagua njia ya uhai au njia ya kifo.
Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Maana, tunajua kwamba Kristo amekwisha fufuliwa kutoka kwa wafu na hafi tena; kifo hakimtawali tena.
Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu.
lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo.
Maana sisi ni kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristo anamtolea Mungu, harufu nzuri inayofikia wote, wanaookolewa na wanaopotea. Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi ya namna hiyo?
Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka kwa wafu kumesababishwa na mtu mmoja.
Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi; na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”
Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.
“Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai.
Paulo, Apolo na Kefa, ulimwengu, maisha na kifo; mambo ya sasa na ya baadaye, yote ni yenu.
Naziita mbingu na dunia zishuhudie juu yenu leo hii, kwamba nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati ya baraka na laana. Basi, chagueni uhai nyinyi na wazawa wenu mpate kuishi,
Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa; ushindi umekamilika!” “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”
Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao, watu ambao wanatumainia fadhili zake. Yeye huwaokoa katika kifo, huwaweka hai wakati wa njaa.
Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo,
Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa!
Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanya kazi.
Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi ya namna hiyo?
Sifurahii kifo cha mtu yeyote. Hivyo tubuni ili mpate kuishi. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
ili apate kuingia kwenye amani.” Watu wanaofuata njia ya haki, watakuwa na amani na kupumzika.
“Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?” Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria. Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka.
Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa;
Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapongolewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
“Mtu ni mtoto tu wa mwanamke; huishi siku chache tena zilizojaa taabu. Lakini mtu hufa na huo ndio mwisho wake. Akisha toa roho anabakiwa na nini tena? “Kama vile maji yakaukavyo ziwani, na mto unavyokoma kutiririka, ndivyo anavyokufa mtu, wala haamki tena; hataamka tena wala kugutuka, hata hapo mbingu zitakapotoweka. “Laiti ungenificha kuzimu; ungenificha hadi ghadhabu yako ipoe; nao muda ulionipimia ukiisha ungenikumbuka. Je, mtu akifa anaweza kuishi tena? Siku zangu zote za kazi ningekungoja hadi wakati wa kufunguliwa ufike. Hapo ungeniita, nami ningeitika, wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako. Ndipo ungeweza kuzihesabu hatua zangu, ungeacha kuzichunguza dhambi zangu. Makosa yangu yangefungiwa katika mfuko, nawe ungeufunika uovu wangu. “Lakini milima huanguka majabali hungoka mahali pake. Mtiririko wa maji hula miamba, mvua kubwa hufanya mmomonyoko wa ardhi. Ndivyo nawe unavyoharibu tumaini la binadamu. Huchanua kama ua, kisha hunyauka. Hukimbia kama kivuli na kutoweka.
“Ee Mwenyezi-Mungu, unijulishe mwisho wangu, siku zangu za kuishi zimenibakia ngapi, nijue yapitavyo kasi maisha yangu!” Kumbe umenipimia maisha mafupi sana! Maisha yangu si kitu mbele yako. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.
Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”
Binadamu akitoa pumzi yake ya mwisho, anarudi mavumbini alimotoka; na hapo mipango yake yote hutoweka.
Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!
maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.
Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la majani. Majani hunyauka na maua huanguka. Lakini neno la Bwana hudumu milele.” Neno hilo ni hiyo Habari Njema mliyohubiriwa.
Najua wazi Mkombozi wangu anaishi, mwishowe yeye atanipa haki yangu hapahapa duniani. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivyo, nitamwona Mungu kwa macho yangu mwenyewe.
Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo, na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwa maisha yao yote kwa sababu ya hofu yao ya kifo.
Mwovu huangamizwa kwa matendo yake maovu, lakini mwadilifu hupata usalama kwa unyofu wake.
Sifa njema ni bora kuliko marashi ya thamani. Siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.
Je, wewe huwatendea wafu maajabu yako? Je, mizimu hufufuka na kukusifu? Je, fadhili zako zinatajwa kaburini, au uaminifu wako kwenye makao ya maangamizi? Je, maajabu yako yanajulikana humo gizani, au wema wako katika nchi ya waliosahauliwa?
Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.
Mtu mwadilifu akifa, hakuna mtu anayejali; mtu mwema akifariki, hakuna mtu anayefikiri na kusema: “Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa, Mlichoshwa na safari zenu ndefu, hata hivyo hamkukata tamaa; mlijipatia nguvu mpya, ndiyo maana hamkuzimia. “Mlimwogopa na kutishwa na nani hata mkasema uongo, mkaacha kunikumbuka mimi na kuacha kabisa kunifikiria? Mimi sikuwaambia kitu kwa muda mrefu; ndio maana labda mkaacha kuniheshimu! Mnafikiri mnafanya sawa, lakini nitayafichua matendo yenu, nayo miungu yenu haitawafaa kitu. Mtakapolia kuomba msaada, rundo la vinyago vyenu na liwaokoe! Upepo utavipeperushia mbali; naam, pumzi itavitupilia mbali. Lakini watakaokimbilia usalama kwangu, wataimiliki nchi, mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Jengeni! Jengeni! Tayarisheni njia! Ondoeni vikwazo vyote njiani mwa watu wangu!” Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa, aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”: “Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu, nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu. Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevu na kuwapa nguvu wenye majuto. Maana sitaendelea kuwalaumu wala kuwakasirikia daima. La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu, nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai. Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe. Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya; nitawaongoza na kuwapa faraja, nitawatuliza hao wanaoomboleza. Mimi nitawapa amani, amani kwa walio mbali na walio karibu! Mimi nitawaponya. ili apate kuingia kwenye amani.” Watu wanaofuata njia ya haki, watakuwa na amani na kupumzika.
Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai.
Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna. Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uhai wa milele.
Siku za kuishi binadamu zimepimwa; ee, Mungu umeipanga idadi ya miezi yake; hawezi kupita kikomo ulichomwekea.