Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


55 Mistari ya Biblia kuhusu Kumtumikia Mungu

55 Mistari ya Biblia kuhusu Kumtumikia Mungu

Rafiki yangu, maisha yetu kama watoto wa Mungu yanapaswa kujikita kwanza kabisa katika kujitoa kwake. Ubora wa huduma yetu unaonyesha yaliyo moyoni mwetu mbele za Mungu na wengine.

Tukizingatia kwamba Mungu alitoa kitu cha thamani kubwa kwetu, anastahili huduma bora iliyojaa shukrani. Katika Biblia, tuna mifano mingi ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu, akifanya matendo ya huduma, si kwa maneno tu, bali pia kwa vitendo mema ndani na nje ya kanisa.

Kwa hivyo, ni muhimu sana kumwiga Yesu kama kielelezo chetu, kufuata nyayo zake na kumwomba msaada na mwongozo ili tuweze kuhudumu kama yeye alivyohudumu. Kwani huduma si kitu kingine bali ni tendo la upendo lenye lengo la kuwafurahisha walio karibu nasi.


Waroma 12:11

Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 12:26

Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 3:9

Maana sisi ni ndugu, wafanyakazi pamoja na Mungu; na nyinyi ni shamba lake; nyinyi ni jengo lake.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:58

Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Samueli 12:24

Basi, nyinyi mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote. Kumbukeni yale mambo makuu aliyowatendea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:1

Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 9:35

Yesu akaketi chini, akawaita wale kumi na wawili, akawaambia, “Mtu akitaka kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 13:14

Basi, ikiwa mimi niliye Bwana na Mwalimu nimewaosha nyinyi miguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Mambo ya Nyakati 28:9

“Nawe Solomoni mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie kwa moyo wako wote na kwa nia thabiti; yeye Mwenyezi-Mungu huchunguza mioyo na anafahamu mipango na fikira za binadamu. Ukimtafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Mambo ya Nyakati 29:9

Ndipo watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa hiari, maana kwa moyo wao wote walimtolea Mwenyezi-Mungu kwa hiari, naye mfalme Daudi alifurahi sana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 2:11

Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji;

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 100:2

Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:21

Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 13:4

Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:10

Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:13

Nyinyi ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 10:27

Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 16:3

Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:25

Mtanitumikia mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nami nitawabariki kwa chakula na maji na kuyaondoa magonjwa kati yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 6:8

Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:24

“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:16

Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 6:10

Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 20:27-28

na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu. Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:35-40

Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha; nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’ Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji? Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’ Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao. Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoshua 24:15

Kama hamtaki kumtumikia Mwenyezi-Mungu, basi chagueni leo hii ni nani mtakayemtumikia: Kwamba ni miungu ile ambayo wazee wenu waliitumikia ngambo ya mto Eufrate, au miungu ya Waamori ambao sasa mnaishi nchini mwao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi-Mungu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoshua 22:5

Muwe waangalifu kutii amri na sheria ambazo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mfuate anachotaka na kushika amri zake; mkae pamoja naye na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:7

Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 10:45

Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:18

Anayemtumikia Kristo namna hiyo humpendeza Mungu, na kukubaliwa na watu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 1:74-75

tukombolewe mikononi mwa maadui zetu, tupate kumtumikia bila hofu, tuwe wanyofu na waadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:22

Mwenyezi-Mungu huokoa maisha ya watumishi wake, wote wanaomkimbilia hawataadhibiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 4:8

Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, na kumtumikia yeye peke yake.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 20:19

Mnajua jinsi nilivyomtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, kwa machozi na matatizo yaliyonipata kutokana na mipango ya hila ya Wayahudi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 84:10

Siku moja tu katika maskani yako, ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali kusimama mlangoni pa nyumba yako, kuliko kuishi nyumbani kwa watu waovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:1-2

Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana. Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia. Ishini kwa kupatana vema nyinyi kwa nyinyi. Msijitakie makuu, bali jishughulisheni na madogo. Msijione kuwa wenye hekima sana. Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote. Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote. Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.” Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:3-4

Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama. Mtu mwadilifu husema maneno ya hekima, kwa ulimi wake hunena yaliyo ya haki. Huizingatia moyoni mwake sheria ya Mungu wake; naye hatetereki katika mwenendo wake. Mtu mwovu humvizia mtu mwema na kujaribu kumuua; lakini Mwenyezi-Mungu hatamtia mtu mwema makuchani mwake, wala kumwacha apatilizwe akishtakiwa. Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kushika njia yake, naye atakukuza uimiliki nchi, na kuwaona waovu wakiangamizwa. Nilimwona mwovu mdhalimu sana, alijiweka juu ya wote kama mierezi ya Lebanoni! Baadaye nikapita hapo, naye hakuwapo tena; nikamtafuta, lakini hakuonekana tena. Mwangalie mtu mwema, mtu mwadilifu; mtu anayependa amani hujaliwa wazawa. Lakini wakosefu wote wataangamizwa; na wazawa wao watafutiliwa mbali. Mwenyezi-Mungu huwaokoa waadilifu, na kuwalinda wakati wa taabu. Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 2:10

Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:7-8

Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu. Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:3-4

Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe. kwani yeye alikuwa hata karibu ya kufa kwa ajili ya kazi ya Kristo, na kuhatarisha maisha yake ili aweze kunipa mimi msaada ule ambao hamkuweza kuuleta nyinyi wenyewe. Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:13

kwani Mungu ndiye afanyaye kazi daima ndani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mpango wake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:23-24

Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 1:9

Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: Jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli,

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:16-18

Furahini daima, salini kila wakati na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 1:12

Namshukuru Bwana wetu Yesu Kristo aliyenipa nguvu kwa ajili ya kazi yangu. Namshukuru kwa kuniona mimi kuwa ni mwaminifu, akaniteua nimtumikie,

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 2:15

Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 9:14

Lakini, kwa damu ya Kristo, mambo makuu zaidi hufanyika! Kwa nguvu ya Roho wa milele, Kristo alijitolea mwenyewe tambiko kamilifu kwa Mungu. Damu yake itatutakasa dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo kifo, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:28

Sisi basi, na tushukuru, kwani tunapokea ufalme usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:22-25

Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo. Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo. Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:10-11

Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine kama wakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 1:5-8

Kwa sababu hiyo, fanyeni bidii ya kuongeza imani yenu kwa fadhila, fadhila yenu kwa elimu, elimu yenu kwa kuwa na kiasi, kuwa na kiasi kwa uvumilivu, uvumilivu wenu kwa uchaji wa Mungu, uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:18

Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 2:19

Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 3:8

Nayajua mambo yako yote! Sasa, nimefungua mbele yako mlango ambao hakuna mtu awezaye kuufunga; najua kwamba ingawa huna nguvu sana, hata hivyo, umelitii neno langu wala hukulikana jina langu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 7:15

Ndiyo maana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungu mchana na usiku katika hekalu lake; naye aketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yao kuwalinda.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu wetu mwema Yesu, wewe u mwema, rehema na upendo wako ni mkuu, unaishi na kutawala milele, kwani ufalme wako hauna mwisho, hautikisiki. Baba, asante, kwa sababu umeahidi kwamba pale wawili au watatu wanapokutana kwa jina lako, hapo ndipo ulipo katikati yetu. Na leo tuko pamoja hapa nyumbani mwako kusifu na kulitukuza jina lako, nakuomba Roho Mtakatifu, uchukue udhibiti wa ibada hii. Uwepo wako ushuke mahali hapa nasi tujazwe na utukufu wako na mara nyingine tena nguvu yako idhihirishwe kupitia miujiza, uponyaji na ukombozi. Nakuomba uimpakae maisha ya mchungaji wetu na umimwagie mafuta mapya na umtumie katika huduma ya neno lako, litakalofundishwa siku ya leo, ili sote tujengwe na kufundishwa ndani yake. Roho Mtakatifu tayarisha mioyo ya kanisa lako, utuamshie njaa na kiu ya neno lako na uwepo wako. Tusaidie kusimama imara katika imani, kudumisha umoja kati ya ndugu na kuendelea katika maombi. Kama vile kanisa la kwanza, ambapo wote walidumu katika mafundisho na ushirika wao kwa wao. Bwana, uwaimarishe maisha ya ndugu zangu, ili katika siku hii ya ibada waweze kufanya kazi yao kwa ubora kwa ajili yako na si kwa ajili ya wanadamu. Asante, kwa ajili ya siku hii ya ibada na zile zijazo. Katika jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo