Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia

- Matangazo -



94 Mistari ya Biblia kuhusu Manabii wa Uongo na udanganyifu wao

94 Mistari ya Biblia kuhusu Manabii wa Uongo na udanganyifu wao


Ufunuo 13:11

Kisha, nikamwona mnyama mwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembe mbili kama pembe za kondoo, na aliongea kama joka.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:12

Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 57:3

Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Njoni hapa nyinyi wana wa wachawi; nyinyi wazawa wa wachawi, wazinzi na malaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 14:15

Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi kuhusu hao manabii wanaotabiri kwa jina langu, ingawa mimi sikuwatuma, na wanaosema kwamba hapatakuwa na vita wala njaa katika nchi hii: Manabii hao wataangamia kwa upanga na kwa njaa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:33

Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 10:2

Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu, na kuwapa watu faraja tupu. Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 13:5

Lakini nabii huyo au mtabiri wa ndoto atauawa, kwa sababu atakuwa amewafundisha uasi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka utumwani, ili muiache njia ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwaamuru muifuatea. Hivyo ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:4

Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:22

Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Kristo. Mtu wa namna hiyo ni mpinzani wa Kristo – anamkana Baba na Mwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:15

“Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi juu ya manabii wa Yerusalemu: Nitawalisha uchungu, na kuwapa maji yenye sumu wanywe. Maana, kutoka kwa manabii wa Yerusalemu kutomcha Mungu kumeenea kila mahali nchini.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 13:6

Maono yao ni ya uongo mtupu na wanachotabiri ni udanganyifu mtupu. Hudai kwamba wanasema kwa niaba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, lakini mimi sikuwatuma; kisha wananitazamia nitimize wanayosema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 28:15

Basi, nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza, Hanania, Mwenyezi-Mungu hakukutuma, nawe unawafanya watu hawa waamini uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 3:5

Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 18:22

Kama nabii akisema kitu ati kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kitu hicho hakifanyiki au hakiwi kweli, jambo hilo hakulisema Mwenyezi-Mungu; nabii amelisema kwa ufidhuli, nanyi msitishwe na jambo hilo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 27:15

Mwenyezi-Mungu anasema: ‘Mimi sikuwatuma manabii hao, bali wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, pamoja na hao manabii wanaowatabirieni uongo.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 56:10

Maana viongozi wao wote ni vipofu; wote hawana akili yoyote. Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka, hulala tu na kuota ndoto, hupenda sana kusinzia!

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 13:22

Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, kwa ajili ya kuwapotosha wateule wa Mungu kama ikiwezekana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 22:25

Wakuu wenu ni kama simba anayenguruma araruapo mawindo yake. Wanaua watu, wanawanyanganya watu mali na johari, na kuongeza idadi ya wajane.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 22:23

Basi, ndivyo ilivyo: Mwenyezi-Mungu amewafanya hawa manabii wako wote waseme uongo. Mwenyezi-Mungu amenena mabaya juu yako!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 16:13

Kisha, nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama na kinywani mwa yule nabii wa uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 28:7

Lakini wako wengine waliolewa divai na kuyumbayumba kwa sababu ya pombe; naam, makuhani na manabii wamelewa mvinyo, wamevurugika kwa divai. Wanayumbayumba kwa pombe kali; maono yao yamepotoka, wanapepesuka katika kutoa hukumu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 16:18

maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 3:5

Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 6:13

Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa, kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali. Tangu manabii hadi makuhani, kila mmoja wao ni mdanganyifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 3:3

Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki nyinyi

Sura   |  Matoleo Nakili
Yuda 1:11

Ole wao! Watu hao wamefuata mwenendo uleule wa Kaini. Kwa ajili ya fedha, wamejiingiza katika mkosi uleule wa Balaamu. Wameasi kama Kora alivyoasi na wameangamizwa kama yeye alivyoangamizwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 28:16

Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu asema kwamba atakuondoa duniani. Mwaka huuhuu utakufa, kwa sababu umewaambia watu wamwasi Mwenyezi-Mungu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:104

Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:12

Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 14:33

Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 2:11

Ndiyo maana Mungu amewaweka chini ya nguvu ya upotovu, wauamini uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 13:3

msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:98

Amri yako iko nami daima, yanipa hekima kuliko maadui zangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:22-23

Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 8:10

Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine, mashamba yao nitawapa wengine. Maana, tangu mdogo hadi mkubwa, kila mmoja ana tamaa ya faida haramu. Tangu manabii hadi makuhani, kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:26

Ole wenu nyinyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 22:27

Viongozi wake waliomo mjini ni kama mbwamwitu wararuao mawindo yao; wanaua ili kujitajirisha visivyo halali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:28

Hali kadhalika nyinyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 3:15

Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 20:29-30

Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo. ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia. Hata kutoka miongoni mwenu watatokea watu ambao watasema mambo ya uongo ili kuwapotosha watu na kuwafanya wawafuate wao tu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:10

Naye Ibilisi aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka madini ya kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 8:44

Nyinyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na hali yake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wa uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 11:3

Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:15-16

“Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 3:13

Watu waovu na wadanganyifu wataendelea kuwa wabaya, wakidanganya wengine, na wao wenyewe wakidanganywa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 12:36

“Basi, nawaambieni, siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:15

“Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 13:1-3

“Akitokea nabii au mtabiri wa ndoto miongoni mwenu, akawaahidi na kuwapa ishara au maajabu fulani, Mpigeni mawe mpaka afe! Kwa sababu amejaribu kukuvutia mbali na Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, aliyekutoa utumwani nchini Misri. Hivyo, Waisraeli wote watasikia na kuogopa, na kamwe hawatafanya uovu kama huo. “Mtakapoishi katika miji ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapa, huenda mkasikia kuwa watu fulani mabaradhuli miongoni mwenu, wamewashawishi watu wa mji wakisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine,’ miungu ambayo bado hamjawahi kuijua, basi mtapeleleza na kufanya uchunguzi na kuuliza kwa makini; na kama ni kweli kuwa jambo la kuchukiza limetendeka kati yenu, hamna budi kuwaua kwa upanga watu wa mji huo; mtauangamiza kabisa mji huo na kuwaua ng'ombe wote kwa upanga. Mtakusanya nyara zake zote katika uwanja wa hadhara wa mji na kuzichoma kwa moto kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wenu; mji huo utakuwa rundo la magofu milele, nao hautajengwa tena. Msichukue kitu chochote kilichotolewa kiteketezwe, ili Mwenyezi-Mungu aache ile hasira yake kali, awaoneshe rehema na huruma, na kuwafanya muwe wengi sana kama alivyowaahidi babu zenu, kama tu mtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkishika amri zake zote ninazowapa hivi leo, na kufanya yaliyo sawa mbele yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. halafu ishara au maajabu hayo yatokee, kisha aseme: ‘Tufuate miungu mingine na kuitumikia, (miungu ambayo hamjapata kuijua)’, msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 13:2

Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, majina ya vinyago vya miungu nchini nitayaondoa, wala hayatakumbukwa tena. Na wanaojidai kuwa manabii nitawaondolea mbali pamoja na tamaa zao za kuabudu sanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 11:4

Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, nyinyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au Injili tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 5:31

Manabii wanatabiri mambo ya uongo, makuhani nao hutafuta faida yao wenyewe; na watu wangu wanaona jambo hilo kuwa sawa. Lakini mwisho utakapofika mtafanyaje?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:21-23

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 22:28

Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mtu anapotia chokaa kwenye ukuta mbovu. Wanaona maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu, wakisema, ‘Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi,’ wakati mimi mwenyewe sijawaambia chochote.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:18

Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 3:11

Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 29:8-9

Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Msikubali kudanganywa na manabii wenu na waaguzi waliomo miongoni mwenu, wala msisikilize ndoto wanazoota. Maana wanawatabiria uongo kwa kutumia jina langu. Mimi sikuwatuma. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:21

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi sikuwatuma hao manabii, lakini wao walikwenda mbio; sikuwaambia kitu chochote, lakini wao walitabiri!

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 4:1

Roho asema waziwazi kwamba siku za baadaye watu wengine wataitupilia mbali imani; watazitii roho danganyifu na kufuata mafundisho ya pepo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 16:17

Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:24

Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 11:13-15

Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu wanaojisingizia kuwa mitume wa Kristo. Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga! Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 14:14

Naye Mwenyezi-Mungu, akaniambia: “Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi yasiyo na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 18:20

Lakini nabii yeyote atakayesema kwa jina la miungu mingine, au atakayejaribu kusema neno kwa jina langu hali mimi sikumwambia aseme, huyo nabii atakufa.’

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:1

Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:16

Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Msisikilize maneno ya manabii wanaowatabiria; wanawapeni matumaini ya uongo. Wanayowaambia ni maono yao wenyewe, wala hayakutoka kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 13:9

Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu nyinyi manabii mnaotoa maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu. Watu wangu watakapokutanika kuamua mambo, nyinyi hamtakuwapo. Wala hamtakuwa katika orodha ya watu wa Israeli na hamtaingia katika nchi ya Israeli; ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:11

Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 4:3-4

Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia. Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 30:10

Huwaambia waonaji: ‘Msione maono’, na manabii: ‘Msitutangazie ukweli, bali tuambieni mambo ya kupendeza, toeni unabii wa mambo ya udanganyifu tu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:3

Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yuko tayari, na Mwangamizi wao yuko macho!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:27-28

“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu. Hali kadhalika nyinyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Sefania 3:4

Manabii wake ni watu wasiojali na wadanganyifu. Makuhani wake wamevitia unajisi vitu vitakatifu na kuihalifu sheria kwa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:3

Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa mpinzani wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 19:20

Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake). Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 13:3

Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Ole wenu manabii wapumbavu mnaofuata mawazo yenu wenyewe na maono yenu wenyewe!

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:11

Mwenyezi-Mungu asema: “Manabii na makuhani, wote hawamchi Mungu, uovu wao nimeuona hata nyumbani mwangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:30

Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawashambulia manabii ambao wanaibiana maneno yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:13

“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Nyinyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie. [

Sura   |  Matoleo Nakili
Yuda 1:4

Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake Kiongozi na Bwana wetu. Lakini, Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu zamani hukumu inayowangojea watu hao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 8:20

Hakika anayesema hivyo hajapata kuona mwanga. Lakini nyinyi shikilieni lile agizo na fundisho la Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 13:6

Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo, upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 2:11

Kama mtu angetokea akatamka maneno matupu ya uongo na kusema: ‘Nawatabirieni divai na pombe kwa wingi’, mhubiri wa namna hiyo angependwa na watu hawa!

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 13:2

“Wewe mtu, wakaripie manabii wa Israeli wanaotangaza mambo ambayo wameyafikiria wao wenyewe. Waambie wasikilize yale ambayo mimi Mwenyezi-Mungu ninasema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 9:15-16

Vichwa ndio wazee na waheshimiwa, mikia ndio manabii wafundishao uongo. Wale wanaoongoza watu hawa wamewapotosha, na hao wanaoongozwa nao wamepotoka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:25

Mimi nimeyasikia maneno waliyosema hao manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, ‘Nimeota ndoto, nimeota ndoto!’

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 15:14

Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 2:14

Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu, hawakufichua wazi uovu wako ili wapate kukurekebisha, bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 6:14

Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu, wanasema; ‘Amani, amani’, kumbe hakuna amani yoyote!

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 2:20

Lakini nina jambo moja dhidi yako: Wewe unamvumilia yule mwanamke Yezebeli anayejiita nabii, anayefundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:32

Naam, mimi Mwenyezi-Mungu nasema kuwa nitawashambulia manabii wanaotabiri ndoto zao za uongo kwa watu wangu, na kuwapotosha kwa uongo wao na kuropoka kwao. Mimi sikuwatuma wala kuwaamuru waende; kwa hiyo hawatawafaa watu hao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wafalme 17:13-14

Mwenyezi-Mungu alituma manabii na waonaji kuionya Israeli na Yuda akisema, “Acheni njia zenu mbaya mkatii amri zangu na maagizo yangu kufuatana na sheria nilizowapa babu zenu, na ambazo niliwapeni kupitia kwa watumishi wangu manabii.” Lakini wao hawakutii; walikuwa wagumu kama babu zao ambao hawakumwamini Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 23:26

Itakuwa hivyo mpaka lini? Hao manabii wataendelea mpaka lini kupotoka moyo; kutabiri uongo na udanganyifu wa mioyo yao wenyewe?

Sura   |  Matoleo Nakili
Tufuate:

Matangazo


Matangazo