Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


100 Mistari ya Biblia kuhusu Kutunza Wazee

100 Mistari ya Biblia kuhusu Kutunza Wazee
Walawi 19:32

“Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 25:8

Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 32:7

Nilisema moyoni: ‘Waache wenye siku nyingi waseme, wenye miaka mingi wafundishe hekima.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:25

Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 46:3-4

“Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo, nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli. Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa; niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu. Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu; hata katika uzee wenu mimi nitawabeba. Nilifanya hivyo kwanza, nitafanya hivyo tena. Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 23:22

Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako akizeeka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 13:1

Mtoto mwenye hekima husikia maagizo ya baba yake, lakini mwenye dharau hasikilizi maonyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ruthu 4:15

Yeye atakurudishia uhai wako na atakutunza katika uzee wako; maana mkwe wako anayekupenda ambaye ana thamani kubwa zaidi kwako kuliko watoto wa kiume saba, ndiye amemzaa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 46:4

Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu; hata katika uzee wenu mimi nitawabeba. Nilifanya hivyo kwanza, nitafanya hivyo tena. Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 5:1-2

Usimkemee mwanamume mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana wa kiume kama ndugu zako, na awe mwenye sifa nzuri: Aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema. Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena, na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali. Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa kusema. Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao ili maadui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juu yetu. Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani. Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa. Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha. Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Usimfunge ng'ombe kinywa anapopura nafaka,” na tena “Mfanyakazi astahili malipo yake.” Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu. wanawake wazee kama mama zako, na vijana wa kike kama dada zako, kwa usafi wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:29-31

Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu. Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 78:5-6

Aliwapa wazawa wa Yakobo masharti, aliweka sheria katika Israeli, ambayo aliwaamuru wazee wetu wawafundishe watoto wao; Aliachilia hasira yake iendelee, wala hakuwaepusha na kifo, bali aliwaangamiza kwa tauni. Aliwaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri; naam, chipukizi wa kwanza kambini mwa Hamu. Kisha aliwahamisha watu wake kama kondoo, akawaongoza jangwani kama kundi la mifugo. Aliwaogoza salama, wala hawakuogopa; lakini bahari iliwafunika maadui zao. Aliwaleta katika nchi yake takatifu, katika mlima aliouteka kwa nguvu yake. Aliyafukuza mataifa mbele yao, akazitoa nchi zao ziwe mali ya Israeli, akayakalisha makabila ya Israeli mahemani mwao. Hata hivyo walimjaribu na kumwasi Mungu Mkuu; wala hawakuzingatia masharti yake. Ila waligeuka na kufanya mabaya kama wazee wao; wakayumbayumba kama upinde usio imara. Walimkasirisha kwa madhabahu zao za miungu; wakamchochea aone wivu kwa sanamu zao za kuchonga. Mungu alipoona hayo, akawaka hasira; akamkataa Israeli katakata. ili watu wa kizazi kijacho, watoto watakaozaliwa baadaye, wazijue, nao pia wawajulishe watoto wao,

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 12:26-27

Kila wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Jambo hili lina maana gani?’ Nyinyi mtawajibu, ‘Hii ni tambiko ya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, kwa sababu alizipita nyumba za Waisraeli nchini Misri alipowaua Wamisri, lakini sisi hakutuua.’” Waisraeli wakainamisha vichwa na kumwabudu Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 12:1

Umkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku na miaka ambapo utasema: “Sifurahii tena vitu hivyo!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 16:31

Kuwa na mvi za uzee ni taji la utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 12:6-7

Baadaye Rehoboamu alitaka kujua maoni ya wazee ambao walikuwa washauri wa baba yake Solomoni, alipokuwa angali hai, akawauliza, “Je, mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?” Wazee hao wakamjibu, “Leo ukiwa mtumishi wa watu hawa, ukawatumikia na kuongea nao vizuri unapowajibu, hapo watakuwa watumishi wako daima.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 20:12

“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 32:9

Si lazima kuwa mzee ili uwe na hekima wala wazee siyo wenye kufahamu lililo sawa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 92:14-15

huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; wapate kutangaza kwamba Mwenyezi-Mungu ni mnyofu, Mwamba wangu, kwake hamna upotovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:7

Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 5:8

Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 23:24

Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha; anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 20:29

Fahari ya vijana ni nguvu zao, uzuri wa vikongwe ni mvi za uzee.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 15:20

Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake, lakini mpumbavu humdharau mama yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 12:12

Hekima iko kwa watu wazee, maarifa kwao walioishi muda mrefu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 19:19

Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 27:16

“ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayemdharau baba yake au mama yake.’ Na watu wote wataitika, ‘Amina!’

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:9

Wakati wa uzee usinitupe; niishiwapo na nguvu usiniache.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 3:7

Kadhalika nanyi waume, katika kuishi na wake zenu mnapaswa kutambua kwamba wao ni dhaifu na hivyo muwatendee kwa heshima; maana nao pia watapokea pamoja nanyi zawadi ya uhai anaowapeni Mungu. Hapo sala zenu hazitatiliwa kizuizi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:1-3

Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara. Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama mkanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu. Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Injili kwa uthabiti. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, Mimi ni balozi kwa ajili ya Injili hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo. Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya. Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo. Ninawatakieni nyinyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho. “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:5

Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Nyinyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 127:3-4

Watoto ni riziki kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; watoto ni tuzo lake kwetu sisi. Watoto waliozaliwa wazazi wakiwa bado vijana, ni kama mishale mikononi mwa askari.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 92:12-14

Waadilifu hustawi kama mitende; hukua kama mierezi ya Lebanoni! Kama miti iliyopandwa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, hustawi katika nyua za Mungu wetu; huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi;

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 7:10

Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?” Huulizi hivyo kwa kutumia hekima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Tito 2:2-3

Waambie wanaume wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu. Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema,

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 12:8

Lakini Rehoboamu alipuuza shauri la wazee; badala yake akashauriana na vijana wa rika lake ambao walikuwa washauri wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 6:20

Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, wala usisahau mafundisho ya mama yako;

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 22:6

Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 32:7

Kumbukeni siku zilizopita, fikirieni miaka ya vizazi vingi; waulizeni baba zenu nao watawajulisha, waulizeni wakubwa wenu nao watawaeleza.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:12-13

Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo. Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:17

Ee Mungu, wewe umenifunza tangu ujana wangu; tena na tena, natangaza matendo yako ya ajabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 19:20

Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 10:7

Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 5:17

Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 10:1

Hizi ni methali za Solomoni: Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake; lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:1-2

Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu, tegeni sikio mpate kuwa na akili. Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu, ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi. Nimekufundisha njia ya hekima, nimekuongoza katika njia nyofu. Ukitembea hatua zako hazitazuiwa, wala ukikimbia hutajikwaa. Zingatia mafundisho ya Hekima na usimwache aponyoke, mshike kwa makini maana yeye ni uhai wako. Usijiingize katika njia ya waovu, wala usifuate mwenendo wa watu wabaya. Iepe njia hiyo wala usiikaribie; jiepushe nayo, uende zako. Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu; hawapati usingizi wasipomkwaza mtu. Maana uovu ndicho chakula chao, ukatili ndiyo divai yao. Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri, ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili. Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae. Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 5:26

Utafariki ukiwa mkongwe mtimilifu, kama mganda wa ngano ya kupurwa iliyoiva vizuri.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 29:8-9

vijana waliponiona walisimama kando, na wazee walisimama wima kwa heshima. Wakuu waliponiona waliacha kuzungumza waliweka mikono juu ya midomo kuwataka watu wakae kimya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:1-2

Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Hapo ghala zako zitajaa nafaka, na mapipa yako yatafurika divai mpya. Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi. Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu. Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu. Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu; kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima. Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 92:14

huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi;

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:20

Umenifanya nione taabu nyingi ngumu, lakini utanirudishia tena uhai, wewe utaniinua tena kutoka huko chini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 90:10

Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 4:16

Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 4:12

Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: Katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 42:16-17

Baada ya hapo, Yobu aliishi miaka 140, akawaona wajukuu na vitukuu vyake vyote hadi kizazi cha nne. Basi, Yobu akafariki akiwa mzee wa miaka mingi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:18

Usiniache, ee Mungu, niwapo mzee mwenye mvi, hata nivitangazie vizazi vijavyo nguvu yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 30:17

Kama mtu akimdhihaki baba yake, na kudharau utii kwa mama yake, kunguru wa bondeni watamdonoa macho, na kuliwa na tai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 15:33

Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima; kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 17:6

Wazee huwaonea fahari wajukuu zao; watoto huwaonea fahari wazazi wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 15:4

Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 15:15

Lakini wewe mwenyewe utaishi maisha marefu na kufariki kwa amani.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 13:4-7

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:13

Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 103:17

Lakini fadhili za Mwenyezi-Mungu hudumu milele, kwa wale wote wanaomheshimu; na wema wake wadumu vizazi vyote,

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:23

Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 1:8-9

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako; hayo yatakupamba kilemba kichwani pako, kama mkufu shingoni mwako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Samueli 12:2

Sasa, mnaye mfalme wa kuwaongoza. Kwa upande wangu, mimi ni mzee mwenye mvi, na watoto wangu wa kiume wako pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu nilipokuwa kijana mpaka sasa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 3:5

Watu watadhulumiana, kila mtu na jirani yake; vijana watawadharau wazee wao, na watu duni watapuuza wakuu wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 2:25

Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoshua 14:10-11

Lakini sasa tazama! Ni muda wa miaka arubaini na mitano tangu Mwenyezi-Mungu alipoongea na Mose, wakati Waisraeli walipokuwa wanapitia jangwani. Tangu wakati huo Mwenyezi-Mungu, kama alivyoahidi, amenihifadhi hai mpaka leo, na sasa mimi nina umri wa miaka themanini na mitano. Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 12:13-14

Mfalme akawajibu watu hao kwa ukali, akapuuza shauri alilopewa na wazee, akafuata shauri la vijana wenzake, akawaambia, “Baba yangu aliwatwika mzigo mzito, lakini mimi nitaufanya kuwa mzito zaidi. Baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa mijeledi yenye miiba.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 78:4

Hatutawaficha watoto wetu; ila tutakisimulia kizazi kijacho matendo matukufu ya Mwenyezi-Mungu na uwezo wake; tutawaambia maajabu yake aliyotenda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:17

‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 19:26-27

Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake, “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” Halafu akamwambia yule mwanafunzi, “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 1:5

Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 12:13

Lakini hekima na uwezo ni vyake Mungu, yeye ana maarifa na ujuzi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 12:15

Mpumbavu huiona njia yake kuwa sawa, lakini mwenye hekima husikiliza shauri.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 22:28

Usiondoe alama ya mipaka ya zamani ambayo iliwekwa na wazee wako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:9

Zaidi ya hayo, sisi tunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hata wanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidi Baba yetu wa kiroho ili tupate kuishi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 4:9

“Lakini muwe waangalifu na kujihadhari sana msije mkasahau mambo yale mliyoyaona kwa macho yenu wenyewe. Isije ikatokea hata mara moja maishani mwenu mambo hayo yakasahaulika mioyoni mwenu. Wasimulieni watoto wenu na wajukuu wenu

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:5-6

Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu; nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu, ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu. Mimi nitakusifu wewe daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:5-6

Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 11:14

Pasipo na uongozi taifa huanguka, penye washauri wengi pana usalama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:4

Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 21:2

Basi, Abrahamu akiwa mzee, Sara akapata mimba, akamzalia mtoto wa kiume, wakati uleule Mungu alioutaja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 48:9

Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wanangu alionijalia Mungu nikiwa huku.” Israeli akasema, “Tafadhali, walete karibu nipate kuwabariki.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 1:6

Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yobu 42:10

Baada ya Yobu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi-Mungu akamrudishia Yobu hali yake ya kwanza. Alimpa maradufu ya yote aliyokuwa nayo hapo awali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 17:1

Wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi-Mungu alimtokea, akamwambia, “Mimi ni Mungu mwenye nguvu. Fuata mwongozo wangu na kuishi bila lawama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:3-4

Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe. kwani yeye alikuwa hata karibu ya kufa kwa ajili ya kazi ya Kristo, na kuhatarisha maisha yake ili aweze kunipa mimi msaada ule ambao hamkuweza kuuleta nyinyi wenyewe. Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mwanzo 45:9

Basi, fanyeni haraka, mwende kwa baba na kumwambia, ‘Yosefu, mwana wako, anasema: Mungu amenifanya kuwa mkuu wa nchi yote ya Misri. Basi, usikawie kuja kwangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 2:36-37

Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:10

Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 103:1-5

Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Yeye hatuadhibu kama tunavyostahili; hatulipizi kadiri ya uovu wetu. Kama vile anga lilivyo juu mbali na dunia, ndivyo ulivyo mwingi wema wake kwa watu wanaomcha. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo azitengavyo dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba amhurumiavyo mwanawe, ndivyo Mwenyezi-Mungu awahurumiavyo wote wamchao. Mungu ajua mfumo wa nafsi zetu; ajua kwamba sisi ni mavumbi. Walakini binadamu, maisha yake ni kama nyasi tu; huchanua kama ua shambani: Upepo huvuma juu yake nalo latoweka; na mahali lilipokuwa hapaonekani tena. Lakini fadhili za Mwenyezi-Mungu hudumu milele, kwa wale wote wanaomheshimu; na wema wake wadumu vizazi vyote, kwa wote wanaozingatia agano lake, wanaokumbuka kutii amri zake. Mwenyezi-Mungu ameweka kiti chake cha enzi mbinguni; yeye anatawala juu ya vitu vyote. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Enyi malaika wakuu, msifuni Mwenyezi-Mungu; mnaotimiza amri zake na kutekeleza neno lake! Enyi jeshi lote la mbinguni, msifuni Mwenyezi-Mungu; enyi watumishi wake mnaotekeleza matakwa yake! Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote; msifuni popote mlipo katika milki yake. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Ndiye anayenisamehe uovu wangu wote, na kuniponya magonjwa yote. Ndiye aniokoaye kutoka kifoni, na kunijalia rehema na fadhili zake. Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote, hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:8

Kinywa changu kimejaa sifa zako, na utukufu wako mchana kutwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 9:10

Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:26

Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 4:13

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hasikilizi shauri jema;

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:2

Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwa wema ili huyo apate kujijenga katika imani.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 12:9

Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Tufuate:

Matangazo


Matangazo