Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 38:8 - Swahili Revised Union Version

8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo,

Tazama sura Nakili




Yobu 38:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.


Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.


Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.


Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango,


Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,


Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.


Hao huziona kazi za BWANA, Na maajabu yake vilindini.


Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala.


Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?


Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;


Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?


Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo