Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 5:13 - Swahili Revised Union Version

13 Ndipo waliteremka mabaki ya waungwana na ya watu; BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wakuu, watu wa Mwenyezi Mungu wakashuka kwangu dhidi ya wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa bwana, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 5:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.


Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.


Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.


Lakini katika mambo hayo yote sisi ni zaidi ya washindi, kupitia kwake yeye aliyetupenda.


Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.


Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.


Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo