Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 9:23 - Swahili Revised Union Version

23 Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; na BWANA akaleta ngurumo na mvua ya mawe, na moto ukashuka juu ya nchi; BWANA akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi yote ya Misri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Basi, Mose alinyosha fimbo yake kuelekea mbinguni. Naye Mwenyezi-Mungu akaleta mvua ya mawe na ngurumo; umeme ukaipiga nchi. Mwenyezi-Mungu alinyesha mvua ya mawe nchini Misri,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Basi, Mose alinyosha fimbo yake kuelekea mbinguni. Naye Mwenyezi-Mungu akaleta mvua ya mawe na ngurumo; umeme ukaipiga nchi. Mwenyezi-Mungu alinyesha mvua ya mawe nchini Misri,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Basi, Mose alinyosha fimbo yake kuelekea mbinguni. Naye Mwenyezi-Mungu akaleta mvua ya mawe na ngurumo; umeme ukaipiga nchi. Mwenyezi-Mungu alinyesha mvua ya mawe nchini Misri,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Musa alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, Mwenyezi Mungu akatuma ngurumo na mvua ya mawe; mwanga wa radi ukamulika hadi nchi. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi ya Misri;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Musa alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, bwana akatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyo bwana akaifanya mvua ya mawe kunyesha juu ya nchi ya Misri,

Tazama sura Nakili




Kutoka 9:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.


Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.


Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?


Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.


BWANA alinguruma kutoka mbinguni, Yeye Aliye Juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto.


Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.


Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;


Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.


Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.


Tazama, kesho wakati kama huu, nitanyesha mvua ya mawe nzito sana, ambayo mfano wake haujakuwa huko Misri tangu siku ile ilipoanza kuwa hata hivi sasa.


Basi palikuwa na mvua ya mawe, na moto uliochanganyikana na ile mvua ya mawe, nzito sana, ambayo mfano wake haukuwapo katika nchi yote ya Misri tangu ilipoanza kuwa taifa.


Naye BWANA atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto uangamizao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu.


Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.


Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa wakiteremka Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hadi kufikia Azeka, nao wakafa; hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga.


Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.


Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.


Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyochangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo