Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 19:9 - Swahili Revised Union Version

9 Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao, wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni. Huko, wakamtia gerezani, ili ngurumo yake isisikike tena juu ya milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao, wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni. Huko, wakamtia gerezani, ili ngurumo yake isisikike tena juu ya milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao, wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni. Huko, wakamtia gerezani, ili ngurumo yake isisikike tena juu ya milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Wakamvutia kwenye tundu kwa kutumia ndoana, wakamleta kwa mfalme wa Babeli. Wakamfunga gerezani, hivyo kunguruma kwake hakukusikika tena katika milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli. Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake hakukusikika tena katika milima ya Israeli.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 19:9
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.


Naye Farao Neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia moja za fedha na talanta ya dhahabu.


Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maofisa wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.


Juu yake akakwea Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamfunga kwa pingu, amchukue mpaka Babeli.


Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.


Akayajua majumba yao, akaiharibu miji yao; nchi ikawa ukiwa, na vyote vilivyomo, kwa sababu ya mshindo wa kunguruma kwake.


Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.


Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli, useme, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la BWANA.


Mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame milima ya Israeli, ukaitabirie,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo