Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 19:17 - Swahili Revised Union Version

17 Ni kweli, BWANA, wafalme wa Ashuru wamewaharibu mataifa na nchi zao,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Ee Mwenyezi-Mungu, ni kweli kwamba wafalme wa Ashuru wameangamiza mataifa na nchi zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Ee Mwenyezi-Mungu, ni kweli kwamba wafalme wa Ashuru wameangamiza mataifa na nchi zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Ee Mwenyezi-Mungu, ni kweli kwamba wafalme wa Ashuru wameangamiza mataifa na nchi zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 “Ni kweli, Ee Mwenyezi Mungu, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “Ni kweli, Ee bwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 19:17
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.


Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.


Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.


Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake wakati wowote na mkono wa mfalme wa Ashuru?


Tega sikio lako, Ee BWANA, usikie; fumbua macho yako, Ee BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai.


na kuitupa miungu yao motoni; kwa maana haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na mawe tu, ndiyo sababu wakaiharibu.


Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.


Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami nitamkatilia mbali kila mwanamume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye asiyefungwa, katika Israeli.


Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru, yaani roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.


Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?


BWANA wa majeshi asema katika masikio yangu, Hakika majumba mengi yatakuwa ukiwa, naam, majumba makubwa, mazuri, yatakuwa hayana watu.


Lakini jueni hakika kwamba, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.


Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.


Nao waliokuwamo ndani ya mashua wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.


Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikazia akisema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yuko kati yenu bila shaka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo