Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 20:29 - Swahili Revised Union Version

29 Wakatua kuelekeana muda wa siku saba. Ikawa siku ya saba vikapangwa vita; wana wa Israeli wakawapiga miongoni mwa Washami siku moja watu laki moja waendao kwa miguu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Watu wa Israeli na Waaramu walipiga kambi kwa muda wa siku saba, wakikabiliana; siku ya saba, mapigano yakaanza. Siku hiyohiyo, watu wa Israeli wakaua askari wa miguu 100,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Watu wa Israeli na Waaramu walipiga kambi kwa muda wa siku saba, wakikabiliana; siku ya saba, mapigano yakaanza. Siku hiyohiyo, watu wa Israeli wakaua askari wa miguu 100,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Watu wa Israeli na Waaramu walipiga kambi kwa muda wa siku saba, wakikabiliana; siku ya saba, mapigano yakaanza. Siku hiyohiyo, watu wa Israeli wakaua askari wa miguu 100,000.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Kwa siku saba walipiga kambi wakitazamana, na siku ya saba vita vikaanza. Waisraeli wakawajeruhi askari wa miguu wa Waaramu wapatao elfu mia moja kwa siku moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Kwa siku saba walipiga kambi wakitazamana na siku ya saba vita vikaanza. Waisraeli wakawajeruhi askari wa miguu wa Waaramu 100,000 kwa siku moja.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 20:29
13 Marejeleo ya Msalaba  

Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.


Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arubaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.


Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, BWANA asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, BWANA ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi BWANA.


Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu elfu ishirini na saba waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.


Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.


Naye Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, akaitwaa tena mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli miji ile aliyoitwaa yeye mkononi mwa Yehoahazi baba yake vitani. Mara tatu Yehoashi akamshinda, akairudisha miji ya Israeli.


Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli elfu mia tano, watu wateule.


Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu elfu mia moja na ishirini, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.


BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa yataangamia kutoka nchi yake.


Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ni siku hiyo tu ambapo waliuzunguka huo mji mara saba.


Kwa siku arubaini yule Mfilisti alijitokeza na kusimama mbele asubuhi na jioni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo