Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wafalme 18:20 - Swahili Revised Union Version

20 Basi, Ahabu akapeleka watu kwa wana wa Israeli wote, akawakusanya manabii pamoja katika mlima wa Karmeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Basi, Ahabu akawaita watu wote wa Israeli, akawakusanya na manabii wote kule mlimani Karmeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Basi, Ahabu akawaita watu wote wa Israeli, akawakusanya na manabii wote kule mlimani Karmeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Basi, Ahabu akawaita watu wote wa Israeli, akawakusanya na manabii wote kule mlimani Karmeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya Mlima Karmeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya mlima Karmeli.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 18:20
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa upeleke watu, unikusanyie jamii ya Israeli katika mlima wa Karmeli, na wale manabii wa Baali mia nne na hamsini, na wale manabii wa Ashera mia nne, walao chakula mezani pa Yezebeli.


Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.


Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.


Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya pamoja manabii, kama watu mia nne. Akawaambia Je! Niende juu ya Ramoth-Gileadi kuupiga vita, au ninyamaze? Wakasema Kwea; kwa kuwa BWANA atautia mkononi mwa mfalme.


Ndipo mfalme wa Israeli akamwita ofisa, akamwambia, mlete hima Mikaya mwana wa Imla.


Akatoka huko akaenda mlima wa Karmeli, na toka huko akarudi mpaka Samaria.


Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo