Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zekaria 6:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Na hayo mataji yatakuwa ya Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; yawe kumbukumbu katika hekalu la BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Taji hilo itahifadhiwa katika hekalu langu kwa heshima ya Heldai, Tobia, Yedaya na Yosia mwana wa Sefania.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Taji hilo itahifadhiwa katika hekalu langu kwa heshima ya Heldai, Tobia, Yedaya na Yosia mwana wa Sefania.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Taji hilo itahifadhiwa katika hekalu langu kwa heshima ya Heldai, Tobia, Yedaya na Yosia mwana wa Sefania.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Taji litatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la bwana.

Tazama sura Nakili




Zekaria 6:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na kamanda wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watu wa mlango;


Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele


Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua majina yao mbele za BWANA juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.


Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya BWANA daima.


Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo nenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli;


naam, pokea fedha na dhahabu, ukatengeneze taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;


viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni yeyote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa kupitia kwa Musa.


Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao makamanda wa maelfu na wa mamia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA.


Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu yake.


Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.


Akamkodolea macho, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.


Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo