Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 91:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji, Na katika maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Hakika Mungu atakuokoa katika mtego; atakukinga na maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Hakika Mungu atakuokoa katika mtego; atakukinga na maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Hakika Mungu atakuokoa katika mtego; atakukinga na maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

Tazama sura Nakili




Zaburi 91:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Basi BWANA akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hadi wakati ulioamriwa; nao wakafa watu elfu sabini toka Dani mpaka Beer-sheba.


Ikiwa kuna njaa katika nchi, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewazingira katika mji wao wowote ule; au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;


Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.


Unilinde kutoka kwa mtego walionitegea, Na kutoka kwa matanzi ya watendao maovu.


Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afululizaye kukosa.


Wala mapigo yajayo usiku, Wala maafa yatokeayo adhuhuri,


Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.


Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.


Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.


Efraimu alikuwa mlinzi pamoja na Mungu wangu; na huyo nabii, mtego wa mwindaji ndege u katika njia zake zote; katika nyumba ya Mungu wake umo uadui.


Je! Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka juu ya nchi, bila kunasa kitu chochote?


Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.


wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo