Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 90:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini? Wahurumie watumishi wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Urudi, ee Mwenyezi-Mungu! Utakasirika hata lini? Utuonee huruma sisi watumishi wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Urudi, ee Mwenyezi-Mungu! Utakasirika hata lini? Utuonee huruma sisi watumishi wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Urudi, ee Mwenyezi-Mungu! Utakasirika hata lini? Utuonee huruma sisi watumishi wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ee Mwenyezi Mungu, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ee bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako.

Tazama sura Nakili




Zaburi 90:13
20 Marejeleo ya Msalaba  

Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;


Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Na kuwahurumia watumishi wake.


Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?


Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele?


Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone, uujie mzabibu huu.


Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako wa kulia; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa imara kwa nafsi yako.


Hadi lini, Ee BWANA? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hadi lini?


Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.


Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.


Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.


Tena itakuwa, baada ya kuwang'oa, nitarudi na kuwahurumia; nami nitawaleta tena, kila mtu aingie katika urithi wake, na kila mtu aingie katika nchi yake.


Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.


BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.


BWANA akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.


Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?


Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.


Tena hapo liliposimama, akasema, Ee BWANA, uwarudie maelfu kumi ya maelfu ya Israeli.


Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo