Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 9:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenyezi-Mungu amejionesha alivyo; ametekeleza hukumu. Watu waovu wamenaswa kwa matendo yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenyezi-Mungu amejionesha alivyo; ametekeleza hukumu. Watu waovu wamenaswa kwa matendo yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenyezi-Mungu amejionesha alivyo; ametekeleza hukumu. Watu waovu wamenaswa kwa matendo yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mwenyezi Mungu anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

Tazama sura Nakili




Zaburi 9:16
26 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.


Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtego utamshika.


Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.


Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike.


Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.


Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.


Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu.


Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.


Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.


Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli walipoangalia nyuma na kuona Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.


Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.


Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.


Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, hapo nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati yao.


Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu.


Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,


Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.


Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.


Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.


Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.


Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo