Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 9:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Wewe, BWANA, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Unirehemu, ee Mwenyezi-Mungu! Ona mateso ninayoteswa na wanaonichukia; wewe waninyakua kutoka nguvu za kifo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Unirehemu, ee Mwenyezi-Mungu! Ona mateso ninayoteswa na wanaonichukia; wewe waninyakua kutoka nguvu za kifo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Unirehemu, ee Mwenyezi-Mungu! Ona mateso ninayoteswa na wanaonichukia; wewe waninyakua kutoka nguvu za kifo,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ee Mwenyezi Mungu, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ee bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

Tazama sura Nakili




Zaburi 9:13
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.


BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?


Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.


Hakika, jana nimeiona damu ya Nabothi, na damu ya wanawe, asema BWANA; nami nitakulipa katika kiwanja hiki, asema BWANA. Basi sasa mtwae huyu ukamtupe katika kiwanja hicho, sawasawa na neno la BWANA.


Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.


Basi sasa, Ee Mungu, mkuu, mwenye uweza, Mungu wa kuogofya, mwenye kushika maagano na rehema, mashaka yote yaliyotupata sisi, wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote, tangu zamani za wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo.


Inuka, Ee Mungu BWANA, uuinue mkono wako, Ee Mungu Usiwasahau wanyonge.


Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.


Unigeukie na kunirehemu, Kama ilivyo desturi yako kwa walipendalo jina lako.


Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako.


Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.


Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.


Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.


Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Na kwa namna wanavyonichukia kwa ukatili mwingi.


Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.


Lakini walio adui zangu bila sababu wana nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.


Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.


Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili niende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.


Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.


Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.


Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.


Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.


Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo