Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 9:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea, wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea, wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea, wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Mwenyezi Mungu, hujawaacha kamwe wanaokutafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.

Tazama sura Nakili




Zaburi 9:10
24 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na kimbilio langu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.


Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.


Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.


Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.


Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.


Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, BWANA, nasema ukweli; nanena mambo ya haki.


Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.


BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.


Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.


Na katika hili tunajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.


Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo