Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 9:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Nitakushukuru Mungu kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Nitakushukuru Mungu kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Nitakushukuru Mungu kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ee Mwenyezi Mungu, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ee bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 9:1
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;


Watangazieni mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.


Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA, Au kuzihubiri sifa zake zote?


Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.


Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.


Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.


Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.


Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.


Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.


Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.


Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.


watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.


Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.


Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.


Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.


Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo