Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 89:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mbingu na zisifu maajabu yako, ee Mwenyezi-Mungu; uaminifu wako usifiwe katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mbingu na zisifu maajabu yako, ee Mwenyezi-Mungu; uaminifu wako usifiwe katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mbingu na zisifu maajabu yako, ee Mwenyezi-Mungu; uaminifu wako usifiwe katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ee Mwenyezi Mungu, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ee bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 89:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako, nitainua mzawa wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitauimarisha ufalme wake.


Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakiimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.


Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?


BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalivunja, Mmoja wa wazawa wako mwenyewe Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.


Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.


Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.


Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.


Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu,


Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni.


Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.


Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake.


Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.


Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.


Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu wakamtumikia, na mamilioni wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.


ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;


Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyaona.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo