Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 89:46 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

46 Hadi lini, Ee BWANA? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hadi lini?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Ee Mwenyezi-Mungu, utajificha hata milele? Hata lini hasira yako itawaka kama moto?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Ee Mwenyezi-Mungu, utajificha hata milele? Hata lini hasira yako itawaka kama moto?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Ee Mwenyezi-Mungu, utajificha hata milele? Hata lini hasira yako itawaka kama moto?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Hata lini, Ee Mwenyezi Mungu? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Hata lini, Ee bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?

Tazama sura Nakili




Zaburi 89:46
17 Marejeleo ya Msalaba  

Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kulia, hata nisimwone.


Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali? Kwani unajificha nyakati za shida?


Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.


Moto ukawala vijana wao, Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,


Ee BWANA, hadi lini? Utaona hasira milele? Wivu wako utawaka kama moto?


Je! Utatufanyia hasira hata milele? Utadumisha ghadhabu kizazi hadi kizazi?


BWANA, kwa nini kuitupa nafsi yangu, Na kunificha uso wako?


Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini? Wahurumie watumishi wako.


Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi.


Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.


Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.


Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.


Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA.


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


katika muali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;


maana Mungu wetu ni moto ulao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo