Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 86:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ee BWANA, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitaji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu, maana mimi ni fukara na mnyonge.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu, maana mimi ni fukara na mnyonge.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu, maana mimi ni fukara na mnyonge.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ee Mwenyezi Mungu, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ee bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.

Tazama sura Nakili




Zaburi 86:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.


Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie.


Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.


Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.


Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.


Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.


Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.


Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.


Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ngome thabiti ya kuniokoa.


Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.


Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.


Tega sikio lako, BWANA, usikie; funua macho yako, BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.


Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.


Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.


Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,


Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo