Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 85:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Mungu wa wokovu wetu, uturudishe, Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Uturekebishe tena, ee Mungu mwokozi wetu; uiondoe chuki uliyo nayo juu yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Uturekebishe tena, ee Mungu mwokozi wetu; uiondoe chuki uliyo nayo juu yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Uturekebishe tena, ee Mungu mwokozi wetu; uiondoe chuki uliyo nayo juu yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 85:4
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Mungu wangu, Nimekutumainia Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.


BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?


Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote.


Ee BWANA, Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Ee Mungu, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Maana bado kitambo kidogo tu ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza.


Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.


Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoea nira; unigeuze, nami nitageuka; kwa maana wewe u BWANA, Mungu wangu.


Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.


Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.


Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitamwangamiza Efraimu tena; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji.


Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.


Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.


Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.


Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata leo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo