Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 81:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mimi ni bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.

Tazama sura Nakili




Zaburi 81:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema.


Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.


Usiwe na miungu mingine ila mimi.


Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;


Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia.


Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.


Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu.


Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.


Usiwe na miungu mingine ila mimi.


Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.


Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.


Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo