Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 73:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kulia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Hata hivyo niko daima nawe, ee Mungu! Wanishika mkono na kunitegemeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Hata hivyo niko daima nawe, ee Mungu! Wanishika mkono na kunitegemeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Hata hivyo niko daima nawe, ee Mungu! Wanishika mkono na kunitegemeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.

Tazama sura Nakili




Zaburi 73:23
14 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.


Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe.


Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.


Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.


Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki.


Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.


Nafsi yangu inaambatana nawe sana; Mkono wako wa kulia unanitegemeza.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.


Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.


Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo