Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 71:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 71:5
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.


Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akiwa bado mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa Maashera, na sanamu za kuchonga, na za kusubu.


Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako, Na maagizo yako nimeyatenda.


Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelitumainia neno lako.


Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.


Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako.


Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.


Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.


Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.


Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, kama mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?


Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.


Usiwe sababu ya hofu kuu kwangu mimi; wewe ndiwe uliye kimbilio langu siku ya uovu.


Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.


Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.


Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.


Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.


na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo