Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 7:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.

Tazama sura Nakili




Zaburi 7:13
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.


Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.


Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale yako, uwafadhaishe.


Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya.


Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme; Watu huanguka chini yako.


Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,


Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake, Na kuwajeruhi ghafla.


Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto.


Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.


Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.


Nitaweka madhara juu yao chungu chungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;


Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.


Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.


Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;


kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.


Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo