Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na asiyetambuliwa na wana wa mama yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:8
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu ya watesi wangu nimelaumiwa, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Wanaoniona njiani wananikimbia.


Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali.


Ambayo adui zako wamesimanga, Ee BWANA, Naam, wamezisimanga hatua za masihi wako.


Na ahimidiwe BWANA milele. Amina na Amina.


Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.


Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.


Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.


Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.


Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.


Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.


Maana hata nduguze hawakumwamini.


Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo