Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, wanaokutumaini wasiaibishwe kwa ajili yangu; wanaokutafuta wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ee Bwana, ewe bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:6
10 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu,


Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.


Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.


Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale.


Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake;


Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.


Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza.


Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi;


Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo