Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Mwenyezi Mungu huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:33
20 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA, utayasikia matakwa ya wanyonge, Uutaidhibiti mioyo yao, utalitega sikio lako.


Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.


Ili akisikie kilio cha kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa.


Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na minyororo,


Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.


Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; BWANA hufungua waliofungwa;


Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.


Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.


Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.


Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.


Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.


Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi;


Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.


Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,


Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;


Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo