Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanazidisha maumivu ya hao uliowatia jeraha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Maana wanawatesa wale uliowaadhibu, wanawaongezea majeraha wale uliowajeruhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Maana wanawatesa wale uliowaadhibu, wanawaongezea majeraha wale uliowajeruhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Maana wanawatesa wale uliowaadhibu, wanawaongezea majeraha wale uliowajeruhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza kuhusu maumivu ya wale uliowaumiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:26
10 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kulikuwako huko nabii wa BWANA, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa BWANA, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni.


Waiharibu njia yangu, Wauzidisha msiba wangu, Watu wasio na msaidizi.


Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo,


Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;


Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.


Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.


Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.


ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wowote;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo