Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini Ee Mwenyezi Mungu, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini Ee bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:13
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.


Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.


Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utatimiziwa.


Mfalme akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta, dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utatimiziwa.


Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye Akuombe awapo katika dhiki. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.


Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.


BWANA asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa;


Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu;


Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao; Wimbo wao ndio mimi.


Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.


Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;


Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]


(Kwa maana asema, Kwa wakati uliokubalika nilikusikia, Na katika siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)


Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;


Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.


Waulize vijana wako, nao watakuambia; basi na wakubaliwe vijana hawa machoni pako; maana tumekujia katika siku ya heri; uwape, nakusihi, chochote kitakachokujia mkononi, uwape watumishi wako na mwanao Daudi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo