Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 69:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa kifani cha dharau kwao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ninapovaa gunia, watu hunidharau.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau.

Tazama sura Nakili




Zaburi 69:11
11 Marejeleo ya Msalaba  

basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.


Amenifanya niwe mithali kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.


Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.


wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.


Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;


Naam, nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana, katika mahali pote nitakapowafukuzia.


Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.


Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili ya mume wa ujana wake.


Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo