Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 64:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hurusha mishale kutoka mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.

Tazama sura Nakili




Zaburi 64:4
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga.


Nao adui zetu wakasema, Hawatajua wala kuona, hadi tutakapokuja kati yao, na kuwaua, na kuikomesha kazi hiyo.


Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.


Mungu atawalaye tangu milele atanisikia; Na kuwaadhibu, maana hawajirekebishi, Wala kumcha Mungu.


Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.


Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.


Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake, Na kuwajeruhi ghafla.


Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.


Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulubishe! Msulubishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulubishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.


Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hadi ukutani. Daudi akaepa, mara mbili.


Sauli akajaribu kumpiga Daudi hadi ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo