Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 61:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa, nikizitekeleza ahadi zangu kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa, nikizitekeleza ahadi zangu kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa, nikizitekeleza ahadi zangu kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

Tazama sura Nakili




Zaburi 61:8
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huku na huko pamoja nasi nami hapa ninaenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe.


Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.


Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.


Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Nami nimevunjika moyo.


Ee Mungu, wastahili sifa katika Sayuni, Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.


Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.


Na sisi tulio watu wako, Na kondoo za malisho yako, Tutakushukuru milele; Tutazisimulia sifa zako kizazi hadi kizazi.


Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo