Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 61:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Nitakaa katika hema yako milele, Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Naomba nikae nyumbani mwako milele nipate usalama chini ya mabawa yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Naomba nikae nyumbani mwako milele nipate usalama chini ya mabawa yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Naomba nikae nyumbani mwako milele nipate usalama chini ya mabawa yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Natamani kukaa kwenye hema lako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mabawa yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

Tazama sura Nakili




Zaburi 61:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu?


Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;


Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.


Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.


Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.


Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.


Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu.


Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.


Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.


Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.


Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.


Waliopandwa katika nyumba ya BWANA Watastawi katika nyua za Mungu wetu.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!


ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo