Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 60:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni chapeo yangu, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

Tazama sura Nakili




Zaburi 60:7
9 Marejeleo ya Msalaba  

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Baadhi ya wana wa Manase walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, tunahatarisha maisha yetu maana atamwangukia bwana wake Sauli.


Tena, ng'ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila la Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, elfu mia moja na ishirini.


Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.


Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.


na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.


Hii ndiyo sehemu waliyopewa kabila la Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Na Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.


Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinzi wangu binafsi daima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo