Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 6:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu! Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu! Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu! Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana bwana amesikia kulia kwangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 6:8
16 Marejeleo ya Msalaba  

Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.


Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka.


Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu.


Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;


BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.


Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.


Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.


Umehesabu kutangatanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)


Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.


akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia kwa uchungu.


Nenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.


Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.


Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;


Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.


Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo