Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 59:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Mwenyezi Mungu, mimi sijakosea wala kutenda dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi.

Tazama sura Nakili




Zaburi 59:3
18 Marejeleo ya Msalaba  

Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huchochea vita.


Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,


Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.


Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa waliniotea ili waniue.


Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.


Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.


Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;


Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.


Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.


Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arubaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hadi watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakisubiri kusikia utasemaje.


Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi.


Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata.


Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya.


Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo