Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 57:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mimi nimezungukwa na maadui, wenye uchu wa damu kama simba; meno yao ni kama mikuki na mishale, ndimi zao ni kama panga kali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mimi nimezungukwa na maadui, wenye uchu wa damu kama simba; meno yao ni kama mikuki na mishale, ndimi zao ni kama panga kali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mimi nimezungukwa na maadui, wenye uchu wa damu kama simba; meno yao ni kama mikuki na mishale, ndimi zao ni kama panga kali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Niko katikati ya simba; nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kali, watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali.

Tazama sura Nakili




Zaburi 57:4
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.


Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.


BWANA, utatazama hadi lini? Uiokoe nafsi yangu kutoka kwa maangamizi yao, Na maisha yangu kutoka kwa wanasimba.


Nitumie nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata katika maskani yako.


Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.


Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.


Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao; Ee BWANA, uyavunje magego ya wanasimba.


Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?


Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.


Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.


Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.


Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.


lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo