Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 55:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imeniingia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Natetemeka kwa hofu kubwa, nimevamiwa na vitisho vikubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Natetemeka kwa hofu kubwa, nimevamiwa na vitisho vikubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Natetemeka kwa hofu kubwa, nimevamiwa na vitisho vikubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha.

Tazama sura Nakili




Zaburi 55:5
12 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga.


Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu.


Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.


Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.


Katika shida yangu nilimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.


Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.


Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.


Moyo wangu unapigapiga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha.


Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.


Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]


Tufuate:

Matangazo


Matangazo