Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 52:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! unafikiria tu kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

Tazama sura Nakili




Zaburi 52:2
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana vinywa viovu na vyenye hila vimefumbuliwa juu yangu, Vikinisema kwa ulimi wa uongo, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.


Ee BWANA, uniponye Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.


Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako unatunga uongo.


Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.


Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.


Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.


Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.


Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;


Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akateremka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza mtawala habari za Paulo.


Kwa maana tumemwona mtu huyu kuwa mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazareti.


Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.


Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.


Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo